Uturuki yazichunia Marekani na Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amesema kuwa nchi yake haichagui Marekani wala Urusi.

Waziri huyo amesema kuwa Uturuki haitofanya chaguo kati ya Marekani na Urusi,Marekani na serikali ya Assad,Ufaransa na Uingereza.

"Lengo letu kuu ni kuleta amani nchini Syria.Hilo ni jambo ambalo Uturuki imelitilia manani",alisema Çavuşoğlu.

Hayo waziri huyo ameyazungumza wakati akitoa hotuba katika mkutano wa chama cha AK mjini Antalya.

Hapo awali waziri Çavuşoğlu alisema kuwa mashambulizi ya Marekani ni dhidi ya serikali ya Assad inayotumia silaha za kemikali.

"Tunapashwa kuikoa Syria kutoka katika serikali hiyo",aliongeza Çavuşoğlu.

Ufaransa,Marekani na Uingereza kwa pamoja zimefanya shambulizi dhidi ya silaha za kemikali za serikali ya Assad nchini Syria.

Hio ni kufuatia shambulizi baya la kemikali lililofanyika Douma na kusababisha vifo vya watu 78 huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa.