F Jinsi ya kutengeneza kashata za nazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Jinsi ya kutengeneza kashata za nazi


Karibu sana mpenzi msomaji wetu wa muungwana blog, nikurike kwa moyo mkunjufu kabisa siku ya leo katika somo hili la kijasiriamali ambapo siku ya leo tutajifunza jinsi ya kutengeneza kashata za nazi.

Mahitaji:
Nazi ilokunwa ya pakti vikombe 3 Changanya na maji kikombe 1 na weka pembeni kama utatumia nazi freshi basi usiweke maji 

Pia unahitaji:
1. Sukari vikombe 2
2. Maji kikombe 1+1/2
3. Rangi ya chakula
4. Hiliki ya unga

Maelekezo:
Tia maji, sukari, rangi na hiliki kwenye sufuria
1. Weka jikoni kiasi cha dakika 7 au zaidi mpaka iwe nzito
2. Kama ulitumia nazi ya pakti weka na maji yake yalobakia
3. Koroga hadi shira ipungue na ianze kujivuta
4. Ukikoroga yote inakuja upande mmoja kama donge na shira yote imeyayuka

Pakaza mafuta chombo chako kisha tumia mwiko kutandaza kashata
Acha ipoe kidogo kisha kata umbo upendalo kisha peleka sokoni.

Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, nakusihi endelea kutembelea blog yetu ya muungwana kila wakati ili uweze kupata masomo kama haya, ambapo sisi huyaita masomo ya pesa mkononi.