Karabai za mafuta huathiri mazalia ya samaki

Na James Timber, Mwanza
Utumiaji wa karabai za mafuta ya taa katika shughuli za uvuvi huchangia kuharibu mazalia ya samaki katika Ziwa Viktoria.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Asasi ya  Wavuvi wadogo Fishers Union Organization jijini hapa  (FUO) Juvenary Matagili amebainisha utumiaji wa karabai hizo humwaga mafuta juu ya maji na samaki hawezi kukaa eneo lenye mafuta.

"Nimekuwa mvuvi kwa muda mrefu nimeona hilo tatizo naomba Serikali kupitia wizara husika waliangalie suala hili na walete njia iliyo bora ambayo itakuwa mbadala kama vile taa za sola, ambazo ni salama zaidi ya karabai," ameeleza Matagili.

Matagili amesema wataalamu ndio wanakwamisha zoezi hilo la utumiaji wa taa za sola kutokana na kutojari afya za watumiaji na kubeza asasi hizo.

Pia amesema kuwa majanga ya moto kwenye kambi za wavuvi mara nyingi huchangia na matumizi ya karabai za mafuta ya taa ambazo nyingine hulipuka na baadhi ya visiwa walipata madhara na kutokana na taa hizo ambapo wengine wakiachwa vilema vya kudumu.

Aidha ameeleza kuwa kilio chake kikubwa ni Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI) baadhi yao wamekuwa wakiwarudisha nyuma na kutowajari mawazo yao mpaka inafikia hatua ya kuwaomba pesa kwa ajili ya utafiti ambapo ni jukumu lao.