Kilimo bora cha pilipili

Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua (angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku).

Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.

Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.

Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu wiki 7 hadi 10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.

Kuhamisha miche shambaini
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea shida yoyote.

MUHIMU...Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia mambo yafuatayo.

Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.

Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho jua limefifia kuepuka miche kukauka.

Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.

Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.

Mahitaji ya mmea
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka.

Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Mau ya mmea hua na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha yenyewe. Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza uchavushaji.

Mbolea
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.

Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka mwisho wa mavuno.

Kupalilia
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia kuepuka kukata mizizi.

Magonjwa
1) Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.

-Ng'oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.

-Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani.

-Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.

-Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.

2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.

Kuepuka / Kuzuia.
-Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
-Mimea iliyoshambuliwa...Ing'oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba.
-Pulizia Ortiva.

3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji ...dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.

Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna choma mabaki yote.
-Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili...badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation)
-Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu...kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu...mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.

4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda....huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.

Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.

Kuepuka.
-Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
-Pulizia dawa yoyote copper.
    
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.

Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .

Kuepuka.
-Nunua mbegu bora
-Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.

NB: Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa

Wadudu waharibifu
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;

A) Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.

B) Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.

Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray...basi weka hizo tray juu ya kichanja.

C) Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.

D) Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.

E) Nematodes na nk.
Tumia solvigo.

Mavuno
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.

Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.

Soko la zao hili
Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.

Changamoto
Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.