F Mbaroni kwa kuiba vifaa vya Mama Samia | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbaroni kwa kuiba vifaa vya Mama Samia


Jeshi la polisi mkoani Dodoma limeendesha msako na kukamata watuhumiwa 19 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo watuhumiwa wa uvunjaji walioiba vifaa vya mafunzo ya TEHAMA vilivyotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan vyenye thamani ya zaidi ya  shilingi Milioni 56 ambapo vifaa hivyo vilitolewa kwa ajili ya mradi maalum wa mafunzo ya tehama nchini

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Gilles Muroto amesema msako huo umekamata watuhumiwa wa makosa ya uvunjaji,watuhumiwa wa kusafirisha madawa ya kulevya pamoja na watuhumiwa wa utapeli ambapo amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakama kujibu tuhuma zinazowakabili.

Aidha katika hatua nyingine Kamanda Muroto amewataka wananchi kutii sheria bila shuruti na kutoa taarifa za wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ambapo amesema mkoa wa Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi hautowavumilia wanaojihusisha na uhalifu.

ITV imezungumza na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma ambapo wameonyesha kusikitisha na vitendo hivyo vya uhalifu huku wakiziomba mamlaka husika kuchukua hatua kali za kisheria kwa wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.