Wito umetolewa kwa waislamu kuwakirimu na kuwatambua waasisi wa mwanzo wa kusomesha na kuhifadhisha Quran tukufu ili kuleta hamasa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameishukuru taasisi ya Al-Hikma kwa kuandaa hafla hiyo ambapo kwa mda mrefu Tanzania imewasahau kuwatambua na kuwathamini waasisi kwani walikua wamesahaulika kwa kipindi chote.
Ameongeza kuwa kwa kitendo cha taasisi hiyo kukubali kuandaa mchakato wa kuandika kitabu cha historia cha waasisi ambao wamekua kioo mpaka sasa ni hatua nzuri na ya kupongezwa kwa dini ya uislamu kwani itaendeleza jamii yenye misingi bora ya imani.
Nae Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema kuwa katika uanzishaji wa kuandika kitabu hicho cha historia ya masheikh waliofanya kazi ya kupigania uisimamia uislamu nchini lazima lazima iwalenge wahusika wakuu na sio kwa matakwa ya waandishi watakao andikika
Pia amesisitiza kuhusiana na vijana wanaohifadhishwa Quran tukufu kuangalia namna ya kuwatunza katika imani kuliko kuachwa huku akitolea mfano mmoja ya mshindi aliechukua tuzo miaka michache iliyopita na leo kuachana na mambo ya dini na kushiriki mambo yasio mpendeza mwenyezimungu.
Ameongeza kuwa katika mashindano mbalimbali yatakayofanyika kwa mara nyingine kuna umuhimu wa kuwaangalia walimu wanaowafundisha ili nao wapate chochote kwani haiwezekani mwanafunzi anapewa gari wakati mwalimu hana hata pikipiki hivyo lazima waangaliwe kwa macho yote