Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kufuatia kuwapo kwa sheria kwa wamiliki wa blogu na majukwaa ya mtandao bila kusahau radio na Televisheni za mtandao kutakwa kujisajili ili kutambulika kisheria. ambapo mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa kwa wale wote ambao hawakuw na leseni kutoka TCRA wajisajili kabla ya tarehe 15/juni/2018 ambapo bada ya hapo sheria zingechukuliwa. Mamlaka hiyo ya mawasiliano TCRA imeongezea muda wa kufanya usaili kutokana na maombi ya wadu waliojitokeza kuomba kuongezewa muda ili kukidhi matakwa ya kisheria. Mamlaka hiyo imeongeza muda hadi kufikia 30/juni/2018.