Msanii wa filamu nchini Irene uwoya amewavaa na kuwajia juu mashabki na wote wanaomfatilia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ya ufukweni akiwa na mavazi ambayo yanaonyesha baadhi ya maungo nyeti ya mwili wake, ambapo iliwafanya mashabiki na baadhi ya wasanii kuchukizwa na kitendo hiko. Hilo lilimfanya msanii huyo kufyatuka maneno mazito na kuwaambia mashabiki kuwa pamoja na yote maneno wanayosema mume wake ameipenda, na kuwasema mashabiki kuwa kila analolifanya yeye huonekana sio jema na kuwataka kuwa akiwa anaposti atawashirikisha.
Kama ulikuwa hujui basi nikujuze kuwa Irene Uwoya ni msanii wa filamu na amefanikiwa kuzaa mtoto mmoja na Mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda na beki wa zamani wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Ndikumana Hamad ambae kwasasa ni marehemu, aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus. na baada ya hapo Irene Uwoya aliamua kuingia kwenye mahusiano mengine na kufunga ndoa na msanii wa muziki tanzania anaeitwa Dogo Janja