Wizara ya utalii yafanikiwa kutatua migogoro


Serikali imesema imeweka mpango kabambe wa kuhakikisha vituo vyote vya utalii vilivyopo hapa nchini  vinatangazwa ili viweze kulinufaisha taifa.

Naibu Waziri wa mali asili na utalii Japhet Hasunga amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo.

Amesema kupitia mkakati huo Wizara hiyo inahitaji ushirikiano wa jamii kuweza kuwaeleza viongozi wa maeneo yao kuhusiana na vivutio vilivyopo maeneo yao ili viweze kutambulika.

Aidha naibu Waziri Hasunga ameliambia bunge kuwa wizara hiyo ya mali asili na utalii imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyokuwepo kati ya wananchi waishio jirani na hifadhi na hifadhi husika.