F Bwege kuomba kibali cha maandamano | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bwege kuomba kibali cha maandamano


Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara ‘Bwege’ amesema kuwa ataenda Jeshi la Polisi kuomba kibali cha maandamano kuhusu madai ya bilioni 201 ambazo zinalalamikiwa kuwa ni fedha kwa ajili ya wakulima wa korosho wa mikoa ya kusini.

Akizungumza kupitia East Africa Breakfast ya East Africa Radio Bwege amesema kuwa wabunge wanaotokea mikoa ya Mtwara na Lindi watakutana na kujadili suala hilo na kuomba kibali cha maandamano.

“kwenye kiasi hicho cha fedha bilioni 201,asilimia 35 ni kwa ajili ya hazina ya serikali na asilimia 65 ni kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya zao la korosho ambapo ingetumika katika kujenga maghala,utafiti,pamoja na kuendeleza viwanda na bila fedha hiyo itakuwa ngumu kuboresha thamani ya zao la korosho” , amesema Bwege.

Aidha Bwege ameongeza kuwa serikali imepitisha sheria hiyo kwa nguvu ikiwemo vitisho lakini msimamo wake uko pale pale kwa kile alichodai kuwa ni kudai haki ya wakulima wa zao la hilo.