F Fei Toto atibua usajili Yanga | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Fei Toto atibua usajili Yanga


Kutua kwa viungo wapya wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Mohamed Issa ‘Banka’ kumemzuia kiungo wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa kutua Jangwani katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Kihimbwa ni kati ya wache­zaji waliokuwepo kwenye mipango ya usajili ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Yanga hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji sita pekee ambao ni Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Jaffary Mohamed, Heritier Makambo, Fei Toto na Banka.

Kwa mujibu wa taarifa am­bazo imezipata Championi Jumatatu, imepata Yanga imemuondoa kiungo huyo katika mipango yao ya usa­jili ni baada ya kukamilisha idadi ya viungo aliyokuwa akihitaji kocha mkuu wa timu hiyo Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Mtoa taarifa huyo al­isema, usajili wao wana­oufanya unatokana na mapendekezo ya kocha mwenyewe katika ripoti ambayo ameikabidhi kwenye kamati ya usajili ya timu hiyo.

“Kihimbwa kwa sasa tumemuweka pembeni na badala yake tunaelekeza usajili wetu katika nafasi ny­ingine ambazo tumepanga kuziboresha ikiwemo safu ya ushambuliaji na ulinzi beki wa kati.

“Juzi tu tulisajili viungo wanne wapya ambao ni Fei Toto, Kaseke, Ngassa na Banka achana na wale wa zamani wenye mikataba, hivyo utaona tuna idadi kubwa ya viungo katika timu.

“Hatutaki kufanya usajili wa hovyo kama wa wale watani wetu, sisi usa­jili wetu tunaufanya kwa kufuata ripoti ya kocha am­bayo ameitoa kwa uongozi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yan­ga, Hussein Nyika, kuzun­gumzia hilo alisema: “Kama uongozi wa Yanga tulifanya na tunafanya mazungumzo na baadhi wachezaji kwa siri kubwa kwa hofu ya wapinzani wetu kutuzidi katika usajili.

“Hivyo, mipango ya kumsajili Kihimbwa hata kama ilikuwepo nisingewe­za kuweka wazi muda huu, kikubwa tusubirie kama atasajiliwa basi tutasema,”alisema Nyika.