Na James Timber, Mwanza,
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amesema hauwezi kushika nafasi ya kwanza kwenye Shindano la Miss Tanzania kama siyo mrembo, tabia yako ni chafu na huna akili timamu.
Mobeto ameyasema hayo baada ya kuteuliwa kwenye kamati ya kuwa mmoja kati ya majaji katika mashindano ya kumchagua Miss Mwanza mwaka huu yatakayofanyika Leo Usiku katika Ukumbi wa Rock City Mall Jijini hapa.
Pia amesema yeye ni kila mwaka anapata nafasi hiyo ya kuwa jaji. "Nashukuru aliyepewa kuwa msimamizi wa Mamis ni Mwanamke kwahiyo sitegemei kama atapendelea lazima achague mtu sahihi na anayefaa kupewa taji hilo bila upendeleo," alisema mobeto.
Aidha Mobeto amesema kuwa yeye ni mzaliwa wa Mwanza, ana heshimu Jiji hili kwa kutoa Warembo anaamini kati ya Mikoa mitano yenye Warembo wa hali ya juu hapa nchini Mkoa wa Mwanza ni miongoni.