Mkwawa alikuwa kiongozi wa jadi wa kabila la wahehe mkoani Iringa nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo.
Miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni ukiachana na chief Mkwawa ni pamoja na Kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora na wengineo.
KUZALIWA
Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 katika kijiji cha LUHOTA nje kidogo na mjini Iringa. Jina halisi aliitwa MKWAVA au MKWAVINYIKA likiwa na maana ya MTAWALA WA NCHI, Mkwawa alikuwa mtoto wa chifu aliyeitwa MUNYIGUMBA aliyekufa mwaka 1879.
Baba yake alifanikiwa kuunganisha temi ndogondogo za wahehe na makabila ya jirani na kuwa dola moja , mfumo huo alinakili toka kwa falme za WASANGU waliowahi kuwa kabila lenye nguvu amabalo mbinu hii pia nao walijifunza toka kwa WANGONI.
Hadi miaka ya 1870 eneo la wahehe lilipanuliwa kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo. Baada ya kifo cha chifu MUNYIGUMBA watoto wake waliingia tofauti kubwa sana katika harakati ya nani achukue madaraka ya hayati baba yao.
Mwisho mkwawa alishinda na akawa kiongozi mpya wa wahehe. Mkwawa aliendelea kupanua dola ya wahehe hadi kufikia mwaka 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na ziwa Tanganyika.
Ambapo misafara hiyo ilikuwa ikibeba bidhaa za nje kama vitambaa, visu, silaha kutoka pwani na ziwa Tanganyika. Misafara hiyo ilipaswa pia kulipa kodi iliyojulikana kama HONGO ambayo iliongezwa uwezo wake nguvu za kijeshi na kiutwala kwa ujumla MKWAWA NA UVAMIZI WA WAJERUMANI Tangu mwaka 1855 hivi, Wajerumani walianza kuunda Koloni lao katika Tanzania bara, Rwanda na Burundi ya leo.
Mnamo mwaka 1891 mkwawa alituma jeshi lake katika kambi ya WAJERUMANI iliyokuwepo mpwapwa na akawaadhibu vibaya wajerumani, sambamba na eneo la USAGARA ambako nako pia alishinda vita dhidi ya wajerumani. Gavana mpya wa kijerumani EMIL VON ZELEWSK alisikia habari za uvamizi wa wahehe, na akaomba kibali cha kuwashambulia wahehe toka BERLIN.
MAPIGANO YA LUGALO
Mwezi julai 1891 Von Zelewsk aliongoza kikosi cha maafisa 13 na askari waafrika kutoka sudani 320 pamoja na wapagazi 113. Walikuwa na bunduki za kisasa na mizinga midogo. Zelewsk aliwadharau wahehe kama washenzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu kwahiyo hakuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali.
Tarehe 17 agosti 1891 Zelewsk na jeshi lake walipita eneo la LUGALO km kadhaa toka Iringa mjini MKWAWA alikuwa akimsubiri akiwa na askari wapatao 3000, Mkwawa aliwashambuliwa wajerumani kwa kushtukiza na dakika kadha wajerumani wengi waliuawa akiwemo kiongozi wao ZELEWSK, wachache kati yao walikimbia ili kujiokoa nafsi zao.
Baada ya vita vya LUGALO mkwawa aliona kuwa wajerumani walikuwa na siraha nzito na muda wowote angewza kupinduliwa hivyo akatuma wajumbe au mabalozi kwa Gavana VON SODEN walioeleza ya kwamba wahehe walikuwa wakijihami tu juu ya mashambulizi ya lugalo na kwahiyo hawakuwa na lengo la kuwaangamiza vile wanaomba maelewano na amani, wajerumani walikubali lakini kwa masharti magumu kuwa misafara ya wafanya biashara ipite kwenye milki yake bila kutzwa HONGO na asishambulie tena vijiji vya jirani zake kwa maana ya kuopanua tena himaya yake.
Mkwawa hakuwa tayari kuahidi yote na hivyo akachelewesha mkutano wa makubaliano hayo, wakati huo kamanda mpya mjerumani TOM VON PRINCE alijenga boma jipya la wajerumani uhehe na MKWAWA alijibu mashambulizi kwa kushambulia vikosi vidogo vya kijeshi vya kikoloni. Gavana SODEN alidai kutoendelea na mapigano lakini mwaka 1893 aliondoka Afrika na gavana von schele alitaka kulipiza kisasi akaa muru mashambulizi dhidi ya mkwawa.
AMANI YA MUDA Mwezi oktoba 1894 Von Schele aliongoza kikosi cha maafisa wajerumani 33 na askari waafrika pamoja na wa pagazi zaidi ya 1000 kuelekea KALENGA. Walipofika mbele ya Kalenga Wahehe walijisikia salama kutokana na kuta imara zilizokuwepo, lakini kutokana na mizinga waliyokuwanayo wajerumani, kuta hizo zilivunjwa kwa mizinga na wakauawa wahehe wengi wakiwemo askari.
Mnamo alfjiri ya tarehe 30 oktoba askari wa jeshi la schtzt ruppe walipanda ukuta katika sehemu iliyodhoofishwa tayari kwa kuingia bomani, mpaka kufika jioni ya siku hiyo mji wote ulikuwa mikononi mwa wajerumani. Mkwawa alikimbia na kujificha mstuni pamoja na askari wa ke. Gavana Von schelle alishindwa kuendelea na mashambulizi kwasababu gharama za uendeshaji wa vita zile zilikuwa kubwa ukilinganisha na makisio aliyoyapeleka Berlin mbali na hilo pia wabunge wa upinzani mjini Berlin walipinga vita za kikoloni na pia wakakataa kuongeza fedha kwa ajili ya vita hizo.
Baada ya kuondoka wajerumani MKWAWA aliweza kurudi na kujenga tena boma katika kijiji cha KALENGA Mnamo sept 1895 Mkwawa alikuwa tayari kujadiliana tena na wajerumani na tarehe 12 oktoba walipata amani na wajerumani walimkubali Mkwawa kama chifu wa wahehe. Wahehe waliahidi kurudisha silaha zote walizoziteka kutoka mikononi mwa wajerumani na kupandisha bendera ya wajerumani kwenye himaya yake vilevile ku waruhusu wafanyabiashara.
Mkwawa alimwagiza mjomba wake kutia saini lakini alikataa kwa madai kuwa hiyo ni sawa na kujiua mwenyewe.
KUANGUKA KWA DOLA YA KIHEHE NA KIFO CHA MKWAWA
Baada ya miezi kadhaa WABENA waliendesha shambulio kali dhidi ya WAHEHE jambo ambalo lilipelekea Wahehe kuomba msaada kwa wajerumani.
Lakini urafiki huu ulidumu kwa muda mfupi sana ambapo afisa mmoja mjerumani alifika KALENGA kwa ajili ya kuonana na chifu Mkwawa lakini alizuiliwa kwa madai ya kulipa HONGO ya bunduki 5 , kwa tukio hilo maafisa wa jeshi la wajerumani waliokuwa wakilinda mpaka ambao bado walikuwa wakitafuta njia ya kulipiza kisasi cha LUGALO wakadai kuwa chifu amevunja makubaliano.
Kapteni wa kijerumani Tom Von Prince alijenga boma jipya karibu na karenga. Baada ya kuona wajeruma ni wamemgeukia Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani zake wakiwemo wabena bila mafanikio, WABENA walikataa katakata hasa walipokumbuka jinsi walivyoshambuliwa na wahehe kipindi cha nyuma. Baadhi ya viongozi wa mkwawa walianza kumsaliti akiwemo mdogo wake aliyeitwa MPANGILE aliyeshikamana na wajeru mani.
Mnamo septemba wahehe waligawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliokuwa wamechoka vita iliku wa tayari kuwakubali wajerumani, wajerumani walimsimika MPANGILE kama chifu mpya wa wahehe lakini baada a ya siku 50 alisimamishwa na kuuawa na wajerumani kwa madi kuwa alikuwa akimsaidia kaka yake kwa siri Kwa kipindi hicho cha mwaka 1896 Mkwawa alikuwa ameondoka IRINGA baada ya kuona mgawanyiko alifuata mkondo wa mto ruaha akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na kumlinda dhidi ya wajerum ani waliokuwa wakimtafuta.
Mnamo Disemba 1896 alihamia milima ya Udzungwa, kutoka huko aliteremka mara kwa mara kwenye mabonde alikopata chakula na kushambulia vikosi vidogo vya askari wa kijerumani. Julai 1897 kikosi kikubwa cha wasangu pamoja na wahehe wakiongozwa na wajerumani walivamia eneo alilokuwa amejificha chifu mkwawa mlimani, lakini mkwawa alikimbia na wakamkosa kwa kipindi hicho.
Julai ya 1898 watu waliokuwa wakimlinda walibaki wachache mno, askari walikuwa 4 pekee, baadaye wakabaki wawili tu ambao majina yake yalipata kufahamika sana MUSIGOMBO na LIFUMIKA, Kwa hofu ya kuuawa na mkwawa LIFUMIKA aliamua kukimbia asubuhi ya tarehe 19, julai lakini hakufika mbali akakutana na wajerumani waliomlazimisha awaambie mkwawa aliko alikataa na baada ya kuadhibiwa sana akawaambia kuwa chifu alikuwa mgonjwa mahali palipo na umbali wa masaa 3.
Walimlazimisha kuwaongoza njiani walisikia muungurumo wa sauti ya risasi 1 wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na kijana mmoja.