Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan ametembelea kiwanda kikubwa cha kuongezea thamani zao la mpunga mradi ambao upo chini ya Kapunga Rice Project Ltd uliopo Mbalari mkoani Mbeya.
Kiwanda hicho kinazalisha tani 22,300 kwa mwaka na wanatumia teknolojia ya kisasa ambapo Kiwanda kina uwezo wa kusafisha mpunga, kukoboa, na kufungasha katika ujazo wa kilo 25, 50, na 100.
Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 100 za mchele kwa siku. Makamu wa Rais anaendelea na ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Mbeya.