Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Charles Mwijage ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Frank Kanyusi ambaye anakuwa mkurugenzi wa pili kutenguliwa wiki hii.
Kutenguliwa kwa Kanyusi kumetokea siku moja baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenister Mhagama, kutengua uteuzi wa Kaimu Mtendaji Mouth wa Wakala wa Huduma za Ajira nchini (TaESA), Saneslaus Chandarua.
Taarifa ya kutenguliwa mkuu huyo wa BRELA haikutaja sababu.
Utenguzi wa Mkurugenzi huyo wa BRELA ulianza jana Julai 20, 2018 ambapo taarifa imesema kuwa tapangiwa kazi nyingine.
Mkurugenzi huyo aliteuliwa mwaka 2014 baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa BRELA kustaafu, hivyo amedumu kwenye nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne.