F Tanzania Prisons kuweka Kambi Zanzibar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Tanzania Prisons kuweka Kambi Zanzibar


Baada ya kumaliza zoezi la majaribio kwa wachezaji watakaoitumikia timu hiyo kwenye ligi kuu msimu ujao,kikosi cha Tanzania Prisons, kinakwenda kuweka kambi visiwani Zanzibar.

Prisons ambayo msimu uliopita ilimaliza kwenye nafasi ya nne imesajili wachezaji watano. Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na wajelajela hao ni Jeremiah Juma pamoja na Kelvin Friday ambaye msimu uliopita alikuwa ni mchezaji wa Mtibwa.

Kwa mujibu wa Championi, Mkuu wa kikosi hicho ambaye pia ndiye kocha bora wa ligi kuu msimu uliyopita Abdallah Mohammed alisema majaribio ya wachezaji yamemsaidia kupata aina ya wachezaji aliyokuwa anawahitaji kwenye kikosi chake.

Pia uongozi wa timu hiyo umewapandisha kikosi cha kwanza wachezaji watano waliyokuwa kwenye kikosi B ambao viwango vyao viko juu.

Kikosi hicho kimeondokewa na wachezaji wao muhimu kwenye eneo la ushambuliaji na kiungo , ambao ni Mohammed Rashid aliyetimkia Simba,Eliuter Mpepo na Kazungu Mashauri wote wamekwenda Singida United.