Je mwenzangu unapenda kunywa soda ngapi kwa siku? Usinipe majibu!
Miongoni kati vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi mara kwa mara ni pamoja na soda ni kwa sababu wafanyabiashara mbalimbali wa vinywaji hivi pamoja na matangazo mengi ya biashara hutangaza kinywaji hivi aina ya soda vinywaji ambavyo hakina madhara kabisa kwa watumiaji wake. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii.
Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kwa sababu maneno yangu sio sheria, lakini ni lazima ukweli nikwambie juu ya vinywaji hivi. Watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya mara baada ya kunywa soda. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe pamoja na sigara, hata kwa wanywa soda ilipaswa kutolewa pia.
Kwani Utafiti unaonesha kuwa soda, pamoja na vikorombwezo vingine, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Na madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili.
Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika. Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako. Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.
watafiti kutoka shule ya tafiti ya harvard wameeleza athari inayoweza kutokea na kuathiri figo kwa wanawake. watafiti hao wameeleza kuwa madhara hayo yanaweza kuwapata wanawake hasa wanapo kunywa soda zaidi ya mara mbili kwa siku. kwani figo huanza kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi wa kawaida. pia wamevihusisha vyakula vyenye sukari nyingi kuwa chanzo cha madhara katika figo.
Mara baada ya kuujua ukweli huu naomba maaumuzi yabaki kuwa kwako.