F Afanya jaribio la kutumbukiza kichanga chake chooni baada ya kujifungua | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Afanya jaribio la kutumbukiza kichanga chake chooni baada ya kujifungua

Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mwanamke anayetambulika kwa jina la Fatuma Abdurhaman,mkazi wa Kilwa Kivinje anadhaniwa kutaka kumtupia chooni mtoto wake baada ya kujifungua.

Kwamujibu wa maelezo ya mama mzazi wa Fatuma,Mwajuma Luwawi kitendo hicho cha kikatili kimefanyika leo asubu.Hata hivyo mama huyo(Mwajuma) aliwahi kumuokoa mtoto huyo kabla hatoswa chooni.

Mwajuma alisema alisikia kilio cha mtoto mchanga chooni,alipokwenda alimkuta Fatuma huku kitoto hicho kikiwa chini karibu na shimo la choo.Hivyo kulazimika kuomba msaada kwa majirani ambao walikwenda na kufanikiwa kuwapeleka kichanga na mama huyo katili katika hospitali ya wilaya Kilwa(Kinyonga).

Kwaupande wake Fatuma alipoulizwa akiwa katika hospitali hiyo ya Kinyonga,kwanini alikwenda kujifungulia eneo lisilo sahihi,alisema akikuwa hajui kama alikuwa na mimba.Japokuwa anamtoto wa mwenye umri wa miaka mitatu.

Fatima katika utetezi wake alisema alipokuwa anakwenda hospitali akikuwa anaambiwa ana vidonda vya tumbo na anadonge tumboni.Kwahiyo hata alipokwenda chooni humo hakujua kama atajwenda kujifungua.

Fatuma alipoulizwa kama hakusikia uchungu kabla na wakati wakujifungua,akisema akikuwa hajisikii uchungu wowote.Kutokana kutohisi kama anamimba kulisababisha asiende kliniki katika kipindi chote cha ujauzito wake.

Kwamujibu wa muuguzi wa zamu katika chumba cha wazazi,Fatuma na mtoto huyo wa kike afya zao ni mzuri.Hatahivyo anaendelea kupata huduma za msingi hospitalini hapo kabla hawajaruhusiwa kuondoka.
 
Alipoulizwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,kamishina msaidizi wa polisi,Pudensiana Protas  kuhusu tukio hilo.Alisema hakuwa na taarifa.Bali atafuatilia ilikujua ukweli wa tukio hilo.

Juhudi za kumpata mganga mkuu wa wilaya ya Kilwa hazikufanikiwa kutokana na mganga huyo kuwa nje ya ofisi.