F Harusi ya muigizaji Mafufu kurushwa 'Live' | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Harusi ya muigizaji Mafufu kurushwa 'Live'

UBUYU ukufikie kuwa, harusi ya mwigizaji mkongwe wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu inatarajiwa kuruka hewani ‘live’ itakapofungwa jijini Dar, Agosti 25, mwaka huu.

Taarifa iliyolifikia Ijumaa Wikienda ilieleza kuwa, shughuli hiyo itarushwa kupitia Televisheni ya Wasafi ikiwa ni sehemu ya kuonesha umuhimu wa ndoa hiyo ambapo Mafufu anaoa kwa mara ya pili baada ya ndoa yake ya kwanza kuota mbawa.

Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mafufu alisema kuwa, ameamua kufanya hivyo kwa sababu yupo tayari kufanyiwa mahojiano yoyote na waandishi wa habari hata kama yatakakuwa yanamhusu yeye na mwanamke wake wa zamani atayajibu ili kila mtu ajue kilichotokea awali.

“Unajua nilipotaka kuoa niliongea na Mungu kupitia njia ya sala na hata sasa siku yangu hii itakuwa ikionekana hatua kwa hatua kwenye televisheni na nipo tayari kuulizwa chochote kinachohusiana na ndoa yangu mpya na hata ile ya zamani.

Mafufu aliongeza kuwa, kikubwa anamshukuru Mungu kwani anatarajia kufunga ndoa na mwanamke ambaye anamjua vizuri tangu wakiwa watoto wadogo na hadi familia zinajuana vyema.