Kiba kuongeza nguvu Coastal Union

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Coastal Union, Ali Kiba Saleh amejiunga na kambi ya timu hiyo huko Tanga.

Kiba anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya KMC Jumamosi ya Septemba 1 saa katika dimba la Mkwakwani Tanga.

Kiba ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi akiwa kama Mwanamuziki kutokana na kufanya vema ikiwa ni pamoja na kutwaa tuzo ya Msanii Bora wa Afrika mwaka 2016, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

Mchezaji huyo alikosa mechi mbili za mwanzo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ambapo alikuwa nchini Canada kwa ajili ya kazi za kimuziki.