F Mtangazaji wa Clouds FM, Diva adai ameambiwa hawezi kupata ujauzito, aomba kuchangiwa milioni 15 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva adai ameambiwa hawezi kupata ujauzito, aomba kuchangiwa milioni 15


Mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Ala za Roho, Diva The Bawse, ameandika barua ndefu yenye ujumbe wa kusikitisha ndani yake akiomba msaada wa kiasi cha dola 7000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya kutungishwa mimba kwa mfumo wa kisasa wa IVF nchini Marekani.

Kupitia barua hiyo mrefu zaidi aliyoiandika kwenye mtandao wa Instagram, Diva, amesema kuwa mwezi uliopita Hospitali ya TMJ kufanya vipimo na aliambiwa kuwa mirija yake ya uzazi ina hitilafu (blockage) hivyo hawezi kutunga mimba kwa njia ya kawaida mpaka kwa mfumo wa kisasa wa kupandikiza mbegu wa IVF Treatment.

Soma barua hiyo hapa chini:

Nitachokiandika ni kitu ambacho kinaumiza sana Moyo wangu , Naandika Machozi yakiwa yananitoka , Sikutaka kuandika lakini Nahitaji kuandika ili nipate msaada zaidi, Sababu haya ni maisha yangu na naandika toka moyoni sitajali mtu atanifikiria nini au atawaza nini, hii situation is confusing sana na ndio maana nimeshindwa hata kulala yan nashindwa kulala kwa ajili ya hii issue sio tu kulala hata kula vizuri siwezi , Moyo wangu una maumivu mengi sana , Nimejiuliza maswali sipati, ila nimeamua kuandika hapa, Kwa muda sasa kama mwaka niliamua kutafuta mtoto, Nimekunywa kila aina ya dawa mnayoijua nyinyi, za hospitali ndio nimemeza mpaka ikafika kipindi nikachoka, hizo za kunywa ndio nimemeza mpaka nimechoka, nikaamua kuchukua likizo kwa ajili ya vipimo very deep kujua tatizo ni nini, In my life nishawahi kupata ujauzito lakini haukufika ata Miezi4 and i lost the baby, kiukweli ilivyotokea mimi mwenyewe nilishang'aa, ila kwa ajili ya mambo yaliyokuwa yanaendelea kwenye hio relationship na huyo mwanaume anaitwa Solomoni frank , niliona labda Mungu ana Mipango yake, too many lies, so i decided to step out n focus on me ,how i met him Sitaki hata kuandika hapa ila iko siku i will share , Hivyo Basi nikakutana na Madaktari wa TMJ hospital nikafanya kipimo kujua kwanini kupata ujauzito inakuwa mtihani sana. sababu vipimo vyote vilikuwa sawa nikaamua kufanya kipimo cha mirija, ambacho nilifanya 9th july 2018. kwa Mtu alieniona hii siku atagundua nilikuwa na maumivu sana , Nililia sana sijawahi lia kama hivyo katika maisha yangu, Nililia sana Nilikuwa na maumivu sina mfano wa kuyafananisha, went to see Dr, Msemo wa Sanitas hosp ambae pia anafanya kazi TMJ ili nijue hasa tatizo , Yeye ni Daktari wangu , Akaniambia majibu yapo umekutwa na Bilateral Cornual Block yaani mirija imeziba, ata kupata mtoto kwa njia ya kawaida inakuwa maajabu sana. alivyokuwa ananielezea Nilijikuta nalia Machozi yana teremka, nilishindwa drive i was in deep pain, nilitamani yule mtoto aliepotea arudi. at some point Sikuwa Pia naamini Mungu ana Exist , historia tu ya maisha yangu ilinifanya nitamani sana mtoto wangu mwenyewe afu the moment nahitaji sana ndio napewa haya majibu.

Basi nilijikuta nalia kupita maelezo ....had to call a friend called @qqtrends4u and gladly she was there for me wakati huu wote alikuwa yeye na @soudybrown ndio walini comfort 😭😭 i was heartbroken , tumeambiwa friends to keep ... hao ndio my friends to keep .. i love them sana sijui hata nieleze vipi hakuna maneno sahihi ya kueleza. 
Mungu Mkali sana Nilisema, Mimi Diva ambae natoa misaada , nasaidia, moyo wangu una utu imekuaje haya mambo yanitokee nilijiuliza sana ... sikuweza kulala wala kula mpaka nililazwa kwa kupata Presha, but Nikaanza kuomba kwa Mungu Nikasema hii ni mara ya mwisho naomba, Nikampigia doctor isaac nikamueleza akaniambia Gods Timing.... mambo yatakuwa sawa, nimeamua kuongea labda kuna wanawake pia wanapitia hii situation , ni situation inaumiza sana na kila ninapokutana na swali utazaa lini nakuwa naumia na hili swali sababu yan mimi Diva hata abortion sifanyi why on earth this imetokea, wakati wa ukuaji wangu nimeumwa sana na tumbo na naumwa sana na tumbo, nishawahi fanyiwa upasuaji, hivyo solution ilikuwa kuwa na mtoto ili tatizo la maumivu makali ya tumbo kuisha , hivyo naweza sema nimepitia machungu mengi in my life but stil leo usiku huu nimeamka na kuamua kuandika hivi nimemuomba sana Mungu nikasema Im going public with this. bila aibu wala uoga na ntasaidia wengine pia wapate msaada ninaohitaji mimi wakati huu sababu najua maumivu yake, naandika hii part 2 chozi au niseme machozi yananitoka. Everything happens for a reason right, i have my best friend called @iammelissa_1 nilikuwa nae kwa simu kwa muda akasema Diva Najua unachopitia, "I know it’s a sensitive subject and sad for you to talk about!
But maybe you should talk about it because you are a great influence in your country and have many fans that are maybe having the same trouble as you 
So you could help them too talking about it " hivyo nikakaa chini na kuamua kuandika Hivi ninavyoandika .. i believe God is real ... nikaamua kufungua a page ntaweka link on inaitwa Gofundme.com na kuanzisha Kampeni inaitwa ' Dreams , Hopes , Wishes . Nia is to have a donation ya $7000 kwa ajili ya ivf treatment in America. Namshukuru Daktari wangu alisema haya....


mayai na kizazi chako vyote viko sawa , but unaweza fanya IVF treatment #ivfjourney nikaamua kuwatafuta madaktari wa nje ya nchi kujua nafanyaje, with the amount of money sababu kuna kuishi huko , kula, kwa siku kadhaa pamoja na kupata sperm donor hivyo hio amount inaweza kutosha. Guys ntaweka link hapo from gofundme , ili kama unaweza uchangie sababu mimi hizo hela sina siwezi danganya, thats alot of money, hivyo link apo juu wil help to support My Campaign called ' Dreams, Hopes, Wishes so that i can have My Miracle Baby baby of my own .... Nahangaika kupata mtoto sasa hivi sababu ndio umri sahihi, sitaki sema how much nafanya kazi , nalala 2 hours too, nikisikia sauti ya yule daktari kichwani au ndotoni naamka usingizi unaisha unakata, imagine nimebeba all this moyoni mwezi mzima uliopita , Natembea na maumivu ya Majibu ya Daktari, ila nashukuru amenieleza vizuri tu Daktari wangu amesema ' Diva Your stil young , you can have it all done just pray , save for the treatment , keep calm n collected ... have faith .... yan wakati wengine wanapata watoto wanatupa, some of us needs alot of money for this treatment , dahhh 😭😭😭😭imagine i even set a baby name , baby room, i so wanted in my life mwaka huu niwe na mtoto 1 tu a baby boy afu mambo yanatokea so fast then huja recover unapata all the news za blockage ..... kumbe zinasumbua sana .. na upasuaji wake nao ni kazi ingine to deal with, kipimo chake tu ni maumivu sijawahi pata ona . ila Nimeandika sababu It is completely sensitive I know but you can imagine the pain i feel everyday. The Pain ambayo wanawake wengine wanapitia, ni ngumu sana .. moyo ni kiza kinene msione mtu anacheka, wanawake tunapitia majaribu mengi sana i dont kno why!... nacheka, nafanya kazi , spend time with my family n friends ... nafanya mambo mengine lakini Moyo wangu umevunjika ... Sina raha ... Niko kwenye huzuni kubwa sana maishani... Naamini Mungu yupo na anasikia kilio changu Maana Nimelia sana mpaka nimechoka nimesali sana 🙏 hivyo Pia naomba Mniombee sana ... thanks💕 love you all 🙏 or you can send the money - Diva Gissele AC/ 3007111473924 Equity Bank, link on bio for Money transfer 🙏

Thank you sana kwa kila anaejitahidi kunifikia , details zote za how to transfer money to my account hizo apo juu ya bio yangu, na nataka nihakikishie watu .. kuziba mirija kunaweza ata sababishwa na uti infection ndogo tu sababu hujui, matatizo haya hukomaa inaweza kuwa hata upasuaji speaking of upasuaji been there kuhusu kupata vimbe tumboni ndio sitaki hata elezea nimetumia dawa hadi nimechoka, mwaka jana na mwaka huu metibu vimbe10 tumboni, i have been at the hospital mpaka nikawa nachoka hata kwenda sasa, Wakati naandika niliandika nikaamua kujitoa to lift up wanawake wote wanaopitia tatizo kama langu , najua wanachopitia sana , tunachekwa, tunasimangwa tunasemwa lakini Therez stil hope, wakati naandika nilijua kabisa kuna watu wataongea a b c d but sikujali na im very proud to say nawakilisha wanawake wote Tanzania East africa worldwide wanaopitia hizi situation, nina vyeti vyote vya madaktari since day 1 mpaka hicho cha mwisho , niliweka kila kitu nikajua kabisa kuna siku ima share this , nina imani kuna wenye uelewa na wasio na uelewa likikukuta au likimkuta ndugu yako utaelewa how painful this situation is , Mil 15 za safari yangu ya ivf treatment naifanya wazi na imani kabisa nitafungua njia za watu wengine wenye kuhitaji mtoto, hasa wakihitaji msaada, hii issue can mentally destroy you inaumiza sana, iknow ivf clinic za Tanzania iknow all that jamani mwezi uliopita ulikuwa ni mimi na simu za hospital zote mnazozijua na ma daktari wote mnaowajua nyinyi, hapa Tanzania $5000 kusema ukweli inakutoka na chances is only 73% thats what i heard hivyo sina hakika sana how many wamefanikiwa, mecheck na hosp za turkey, Japan, america, london yan all of them na nimepata best hospital so far, Im gon try . I pray to Allah ... as a celebrity to go on public na kuongea kitu kama hivi sio kitu kidogo naumia sana nalia daily ... ujue maumivu yake ni makali sana na anahitaji msaada regardless..after writing this sitarajii swali la utazaa lini, natarajia kuombeana kwa Mungu nifanikiwe safari yangu ya kutafuta mtoto wangu mwenyewe bila complications tena , hivyo tuombeane mema sababu hilo swali linaumiza sana, Hivyo pls if umeguswa pls help🙏