F Adamu Malima awapa salamu hizi Simba na Yanga | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Adamu Malima awapa salamu hizi Simba na Yanga

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima ambaye pia ni mlezi wa klabu ya Biashara United ya mkoani humo amejigamba kuwa klabu yake haijabahatisha kutoa suluhu na Azam Fc nyumbani na kuzipa salamu Simba na Yanga kuwa zijiandae kupokea kichapo kwa timu hiyo.

Akizungumza kuhusiana na matokeo ya mchezo huo dhidi ya Azam Fc, mkuu huyo wa mkoa amesema,

“Kwa mpira huu wa leo (jana) nyie wenyewe mmejionea kuwa vipaji vipo vingi hadi huku mashambani pembezoni kabisa mwa nchi, hii leo imekuwa kwa Azam Fc lakini wakija Yanga hapa wenyewe ndiyo kabisa hawatoki, angalau Simba kidogo watatoka almanusura ”.

“Mimi nina imani zaidi na timu yangu kwasababu lengo letu mwaka huu sio kuwa mabingwa wa ligi kuu, ila ni kusimama katikati na kuendelea kujijenga kama timu ya ligi kuu, ninachopenda kuwaambia ni kwamba hatuwezi kuwa na ligi yenye timu tatu pekee (Simba, Azam,na Yanga), lazima timu ziongezeke ”, ameongeza mkuu huyo wa mkoa.

Biashara United ina wastani wa alama moja katika kila mchezo waliocheza mpaka sasa, ikiwa na alama tano katika michezo yake mitano. Inakamata nafasi ya kumi nan ne ya msimamo wa ligi kuu.

Yanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union usiku wa jana, inaongoza ligi ikiwa na alama tisa katika michezo yake mitatu iliyoshuka dimbani sawa na JKT Tanzania yenye alama hizo katika michezo yake mitano iliyocheza.