F Hizi ndizo Dalili za awali za kuharibika kwa Mimba | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hizi ndizo Dalili za awali za kuharibika kwa Mimba


Leo tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa kupata watoto.

Kuna wengine wanapata watoto au mtoto mmoja na baadaye wanashindwa kupata mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.

Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika, najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka au huaribika kabla wao hawajagundua kama walikuwa wajawazito.

Isipokuwa wale ambao hujua kwamba walikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zao zimeharibika au walikuwa wajawazito.

Kwa maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na umekuwa haupati lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa mara kadhaa halafu hedhi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.

Dalili za kuharibika kwa mimba
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20.

Na dalili hizo ni kama;

Damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito na bado unaona damu inatoka kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo cha afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba (miscarriage) huwa hakutokei ghafla tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.

kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito
Wakati mwingine  mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu nyepesi na kabla hajatahamaki, damu ile nzito inaanza kutoka tena, na hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi na kuna uwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema zaidi kufuata ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.

Uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo.
kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni changa na unapatwa na maumivu makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako usitoke au usikumbwe na tatizo hili la kutokwa na ujauzito (miscarriage).

Kama unapatwa na dalili kama hizi kutokwa na damu nyepesi au nzito ilihali wewe ni mjamzito basi ni vema kuwahi kituo cha afya au wasiliana nasi ili kukusaidia. Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.