NA TIMOTHY ITEMBE TARIME.
NAIBU Waziri wa madini j,Doto Biteko jana ametatua mgogoro wa madini uliokuwepo wa mda mrefu baina ya wachimbaji wadogowadogo kati ya mmiliki wa leseni,Chacha Wambura katika kijiji cha Mosege kata ya Nyarukoba hamashauri ya Mji wa Tarime vijijini mkoani Mara.
Biteko alisema kuwa katika mgogoro huo amebaini kuwa mmiliki wa leseni ya kuchimba madini ya dhahabu Chacha Wambura walikubaliana na wachimbaji wadogo wadogo hao mambo kadhaa ambapo Wambura alikwepa kusaini mikataba ya makubaliano yao na kisha kujitenga na makubaliano hayo.
"Mimi nimekuja kutatua mgogoro na sitarajii mgogoro huu kuwendelea kuwepo nakuomba kwenda kusaini makubaliano mliokuwa mmekubaliana mbele ya muu wa wilaya,Glorius Luoga kwa kuzingatia kuwa watu wengi ambao wanategemea madini ya dhahabu kaeneo haya hawawezi kutaabika kwaajili ya mtu kwa hali hiyo nenda ukasaini mikataba mliokubaliana mbele ya mkuu wa wilaya Tarime,Glorius Luoga"alisema Biteko.
Naibu waziri aliagiza wachimbaji wadogo wadogo pamoja na mwenye leseni kulipa ushuru wa serikali kwanza kwa kila kinachozalishwa hao ndipo waanze kugawana kwa kuzingatia asilimia 40 ya mwenye leseni na asilimia 60 ya wachimbaji wadogo wadogo.
Kwa upande wake Chacha Wambura alisema kuwa atazingatia maamuzi ya Naibu waziri na kuwa katika mgodi huo hali ilikuwa imechafuka kisai kwamba akitaka kwenda hapo lazima asindiiizwe na polisi kwa uslama wake"Ndugu Naibu Waziri usalama wangu hapa ni mdogo kwasbabu jamii ya wakazi wa hapa ni koo moja nami ni koo ya Tarime kwa hali hiyo wananichukia hata wafanyakazi wangu wanaishi katika mazingira magumu"alisema Chacha.
Diwani kata ya Nyarukoba,Matiko Bisendo alimwambia Naibi waziri huyo kuwa Chacha ni muongo kwasababu wakazi wa hapo wanalinda mashine zake ambazo asilimia kubwa ndizo zizofanya kazi ya kuvuta maji,kuchoronga na kusaga mawe"kama anasema kuwa watu wa hapo wanamchukia kwasababu ya koo ni uongo mbona hawajaharibu hizo mashine"alisema Bisendo.
Pia diwani huyo aliongeza kuwa mwenye leseni halipi ushuru wa halmashauri kwamaana ya Savece Levy pia amechukua makabi ya mchanga yenye dhamani ya shilingi milioni 90 na kukimbia nayo kusiko julikana buila kuwalipa hata ushuru wa kijiji.