F "Sijaandika barua ya kutaka kujiuzuru" Kubenea | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

"Sijaandika barua ya kutaka kujiuzuru" Kubenea


Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Saed Kubenea amesema hajaandika barua yeyote ya kutaka kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani kama ilivyokua ikisambaa hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii.

 Akizungumza na akiwa njiani kuelekea kwenye ufungaji wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Monduli Kubenea amesema hajaandika barua yeyote  badala yake anaiona kupitia mitandao ya kijamii na kuongeza pia hajapokea barua yeyote kutoka kwa viongozi wa Chama chake ikimtaka kujieleza kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu

“Mimi sijui kuhusu hiyo barua na wala sijaiona .., kuhusu kuandikiwa barua na katibu mkuu mimi sijaiona na kama ipo haijanifikia", amesema Kubenea

Kupitia  mkutano wa na waandishi wa habari Katibu mkuu wa Chama cha  Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  Dk. Vincent Mashinji alikiri kuona barua ya mbunge huyo kupitia mitandao ya kijamii, huku akiweka wazi kwamba pindi itakapomfikia ataifanyia kazi.

Hivi karibuni Mgombea Jimbo la Ukonga Mwita Waitara alisema watarajie jambo lolote juu  ya hatma ya Mbunge huyo wa Ubungo Saed Kubenea ndani ya CHADEMA.