F BREAKING: Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa amekamatwa na polisi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

BREAKING: Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa amekamatwa na polisi


Na.Ahmad Mmow,Lindi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi,Abou  Mussa Mjaka amekamatwa na jeshi la polisi.

Taarifa kutoka wilayani humo zinaeleza mheshimiwa Mjaka alikamatwa jana majira ya saa nne usiku nyumbani kwake mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Taarifa hizo ambazo zimethibitishwa na mkuu wa wilàya ya Kilwa,Christopher Ngubiagai zimeeleza kwamba diwani huyo wa kata ya Masoko(CUF) anatuhumiwa kukutwa na vipande vya mbao takribani  400 ambazo vimevunwa kinyume cha sheria.

"Huyo mheshimiwa nikweli amekatwa usiku huu.Yupo kituo cha polisi cha Kilwa Masoko.Inasemekana amekutwa na mbao takribani 400 ambazo zilikuwa nyumbani kwake.Lakini hakuonesha nyaraka zinazoonesha kuwa nihalali," alisema mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilwa.

Alipoulizwa mwenyekiti wa CUF wa wilaya ya Kilwa,Seleman Bungara(Bwege) alisema hata yeye amesikia.Hata hajui kwa undani kuhusu jambo hilo.Keasababu yeye anaishi Kilwa Kivinje,wakati Mjaka anaishi Kilwa Masoko.

Juhuhudi za kumpata kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Kamishina msaidizi wa Polisi ACP, Pudensiana Protas hazikuzaa matunda.Kwani simu yake iliita bila kupokelewa.Huku mkurugenzi wa siasa,uenezi na itikadi wa CUF wilaya ya Kilwa,Deo Chaurembo hakupatika na hewani.

Halmashauri ya wilaya ya Kilwa ipo chini ya chama cha CUF kutokana na wingi wa madiwani wansotokana na chama hicho.Huku majimbo yote mawili(Kilwa kusini na kasikazini) wabunge wake wanatokana na chama hicho pia.