Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya amesema kuwa hawezi kuwekeza fedha nyingi kwenye kutengeneza video kwani nyingi kwa sasa hazifanyi vizuri.
Dudu Baya amesema hayo kwenye mahojiano na Muungana TV ambapo amewataja wasanii kama Shilole, Jux na Weusi video zao kutofanya vizuri kama hapo awali.
"Weusi wana video karibia sita hazijafikia malengo kama ilivyokuwa Weusi kwa kipindi kile. Ukiangalia video za wasanii wengi sana kina Shilole, Jux hazijafikia malengo na hata wao wanakiri hajazijafikia malengo," amesema Dudu Baya.