Yaelezwa kuwa kiungo wa klabu ya Yanga, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto amesema kung'ara kwa Simba juzi Taifa dhidi yao ni kutokana na mbinu alizotumia kocha wao.
Toto amesema kuwa Simba walikuwa wazuri zaidi haswa kwenye nafasi ya kiungo baada ya Kocha wao, Mwinyi Zahera kuwataka wasicheze kwa kushambulia.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka JKU ya Zanzibar amefunguka kuwa Zahera aliwapa mbinu ya kucheza huku wakijilinda ili kuepusha kuwapa nafasi ya upenyo wapinzani wao.
Safu hiyo ya kiungo iliyokuwa ikiongozwa na Jonas Mkude, Mgahana James Kotei na Mzambia Clatous Chama ilikuwa chachu ya Simba kuweza kuwashambulia zaidi Yanga.
Katika mechi hiyo, Simba na Yanga zilimaliza mchezo kwa matokeo ya bila kufungana (0-0).