F Lava Lava aeleza kwanini Mbosso pekee | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Lava Lava aeleza kwanini Mbosso pekee

Msanii wa muziki Bongo, Lava Lava ameeleza sababu ya kuwa karibu zaidi na Mbosso kuliko wasanii wote wa WCB.

Muimbaji huyo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM ameeleza kuwa hilo linatokana na kuwa walifahamiana kabla ya kuingia WCB.

"Mbosso nimekutana naye kabla sijawa na ndoto za kuwa WCB, nishakutana nao Yamoto Band kama haijatoka na mtu ambaye nilikuwa nimemkubali mara ya kwanza alikuwa ni Mbosso," amesema Mbosso.

Mbosso na Lava Lava amepishana mwaka mmoja kuingia WCB, May 23, 2017 ndipo Lava Lava alitangazwa kuwepo chini ya label ya WCB  wakati usiku wa  January 27, 2018 Mbosso naye akatambulishwa.