Mr. II 'Sugu ambaye ana histori kubwa sana kwenye muziki wa Bongo Fleva hasa kwa upande wa hip hop ameeleza kuwa picha hiyo ni kwa ajili ya cover la kitabu chake kipya.
Mtu yeyote mwenye picha yangu nikiwa nimevaa sare za MFUNGWA tuwasiliane, inahitajika kwa ajili ya cover la KITABU changu kipya 'SIASA NA MAISHA; FROM PARLIAMENT TO PRISON' . Na ZAWADI ya Tsh 1,000,000/= itatolewa kwa atakayeleta picha nzuri itakayotumikaUtakumbuka kuwa Mr. II 'Sugu' Sugu aliachiwa huru May 10, 2018 baada kutumikia kifungo jela kwa zaidi ya miezi minne. Alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli.