F Ongeza Kipato Kwa Kilimo Bora cha Viazi Mviringo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ongeza Kipato Kwa Kilimo Bora cha Viazi Mviringo


Viazi mviringo au kwa jina jingine viazi ulaya ni jina ambalo hutumika kutofautisha zao hili na zao la viazi vitamu. Zao hili ni muhimu kati ya mazao ya mizizi katika maeneo ya miinuko ya Afrika mashariki.

Katika maeneo ya miinuko zaidi, zao hili huwa na mavuno makubwa zaidi kwa zao la mahindi na hukua kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Viazi mviringo hutumika sana kama zao kuu la chakula hapa nchini na pia husafirishwa katika maeneo ya mbali kama vila Kampala, Mombasa na Dar,es salaam.

Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Moshi, Arusha, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile Njombe mkoani Iringa na wilaya za mkoa wa Mbeya.Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.

II. MMEA WA KIAZI ULIVYO
Kiazi ni mzizi wa mmea unaovimba ukiwa chini ya ardhi na kuwa na vijicho vingi, ambavyo baada ya miezi 2 – 3 vijicho hivi huchipua na kuota shina, kijicho kimoja huweza kutoa zaidi ya shina 1 ambapo hutoa vitawi vingine.

Pingili zilizopo kwenye shina hutoa mizizi inayomea chni ya ardhi na miisho yake huvimba na kuwa kiazi. Viazi nyenye ngozi nyeupe huwa na maua meupe na ileyenye rangi hutoa maua ya rangi aidha pinki, bluuau zambarau.Katika mzunguko wa ukuaji kiazi huendelea kukua hata baada ya maua kutoka; ili mradi kuwe na na unyevunyevu wa kutosha kwenye udongo na yasiwepo magonjwa.

II. HALI YA HEWA
Mvua:- Viazi huhitaji mvua za kiasi cha sentimita 25 kwa wiki ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii huweza kukuza viazi na kupata mavuno mazuri.

Joto
Viazi hukua vizuri zaidi kwenye baridi kwa mwinuko wa mita 1,800 kulikoni kwenye joto. Maeneo machache ya mwinuko wa mita 1,500 huweza kukuza viazi, japo pia hukua kwenye mwinuko wa mita 2,900.

Udongo
Viazi hutoa mavuno mazuri kwenye udongo usiokuwa mzito na unaopitisha maji kwa urahisi. Udongo wenye viini lishe vya kutosha au kuongeza samadi na mbolea za viwandani.

IV. AINA ZA VIAZI
Aina zote za viazi zimeingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.
Dutch Robijn - kutoka Holland

  • - ndani ni njano
  • - inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu
  • - hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria
  • - hupendwa na walaji wengi
  • ii. Roslin - kutoka Scotlland
  • - ngozi yake ni nyeupe
  • - ndani ni nyeupe
  • - huvumulia ugonjwa wa ukungu
  • iii. Kerr’s Pink - ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
  • - ndani ni nyeupe
  • - hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria
  • iv. Atzimba - kutoka Mexico
  • - huvumilia ugonjwa wa ukungu

V. MBEGU ZAKUZALISHA VIAZI
Viazi vyenye umbile dogo hutumika kama mbegu, hutakiwa kuwa na upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za tani huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1.
Mbegu hazitakiwi kuhifadhiwa kwenye giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.

VI. KUANDAA SHAMBA
Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hiihusaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi.
Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka.

VII. KUOTESHA VIAZI
Viazi hutakiwa kuoteshwa mara karibu kabisa na mvua zinapotaka kuanza kuchelewa kuotesha kutapunguza kipindi cha ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo kukabiliwa na kipindi cha ukavu.
Uoteshaji hufanyika kwa mikono na mbegu ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10. Kama mbegu zitaoteshwa bila matuta basi zioteshwe kwa kina cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo mchache na wakati wa palizi udongo utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa wingi. Nafasi ya kuotesha ni sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita 23 – 30kwa mche hadi mche.

VIII. MBOLEA
Viazi hustawi vizuri zidi kwenye udongo ulioongezwa samadi na ni muhimu chimbiwe katika kina kirefu. Mbolea za viwandani zinazotakiwa ni zile zenye Nitrogeni kwa kiasi cha kilo 22 – 45 kwa ekari; zenye Chokaa P2O5 kwakilo 45 – 65 kwa ekari.
Ni vyema kuongeza mbolea na samadi wakati kuna mategemeo mazuri ya mavuno kwa kuzingatia kuwa mbegu zilizooteshwa hazina magonjwa ya aina yoyote.

IX. PALIZI
Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi yote na hivyo kugandamiza magugu, hii husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa ni kuondoa magugu na kujaza udongo kwenye mashina.

X. KUVUNA
Uvunaji wa viazi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono, viazi vikishang’olewa kutoka chini ya udongo visiachwe kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa kijani.
Ili kuifanya ngozi yaviazi kuwa ngumu na isiharibike kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya kuvuta viazi juu ya udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwani huanza kuchipua. Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini si zaidi ya wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo fundo.

XI. MAVUNO
Mavuno huwa mengi kama utunzaji wa kitaalamu umezingatiwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti magonjwa, kutumia aina zinazostahimili magonjwa. Kiasi cha tani 6 – 8 kwa ekari huvunwa,sawa na tani 15 – 20 kwa hekta.

KUHIFADHI:-
Uhifadhi wa zao hili ni mgumu, hivyo inashauriwa kuwa sehemu iliyotengwa kwa biashara iuzwe mapema, sehemu ya kutumia nyumbani ihifadhiwe katika banda au ghala safi lenye sakafu, lisilo na unyevu, mwanga wala joto- liwe na hewa safi na ya kutosha. Vinginevyo husababisha viazi kuota haraka. Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa kina kirefu, visambazwe ili visipate joto.

XII. WADUDU
Vidukari:-
Ni wadudu wadogo wanoshambilia majani na mashina kwa:

  • - kufyonza utomvu na kusababisha kunyauka kwa mmea.
  • - Majani kujikunja kuelekea juu.
  • - Majani kuwa magumu
  • - Mimea kudumaa
  • - Pia hubeba vimelea aina ya virusi ambao huathiri mimea.
  • - Pia hueneza ugonjwa wa virus.

Tiba:- Wakati wa utunzaji wa mbegu za viazi ni muhimu kupiga dawa ya wadudu ili kuepuka kupuliza shambani kwani dawa nyingi itapotea.

Nondo wa viazi:-
Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa wakati ambao sio wa msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi na kusababisha kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.

Kuzuia:-

  • Otesha viazi katika kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3 kwani kiwavi
  • aingiae ndani ya hawezi kuchimba kina kirefu na inulia matuta wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo kutaga mayai.
  • Viazi vyote vilivyochimbwa ni muhimu viwekwe kwenye mifuko na mapema kabla ya alasiri ili kuepuka nondo kutaga mayai.
  • Vikihifadhiwa stoo majani ya aina ya LANTANA CAMARA yaweza kutumika.


Tiba:- 

  • Wakati viazi vikiwa stoo, dawa ya unga ya Aldrin hutumika kwenye viazi vya mbegu.
  • Nyunyizia majani ya viazi wakati mmea ukiwa na mwezi 1dawa aina ya Dipterex, Diazon, Thiodan, Permethrin, ACtellic au Sumithion.
  • Kama ni viazi vya kula basi tumia PYRETHRUM.


Minyoofundoo:-
Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa muda mrefu ardhini na kwenye ardhi iliyoathirika na mmomonyoko.

Kuzuia:-

  • - Usioteshe mbegu ambazo zimeshambuliwa na wadudu.
  • - Andaa shamba mapema ili masalia yote ya mazao yaweze kuoza ili kutoruhusu makazi ya minyoo fundo.

Mbawakavu:-
Ni wadudu wadogo ambao hutafuna majani na kuacha matundu matundu.
Kuzuia: Tumia dawa aina ya Malathion, Thiodan

MUHIMU:-
Pamoja madhara ya wadudu pia hueneza magonjwa mbali mbali ya mimea, hivyo kutunza shamba kuwa safi hasa kupalilia; kuchimba na kutupa mbali maotea pamoja na masalia yote na kubadilisha viazi na vipando kama maharage, mahindi, hupunguza madhara.