F Shirika la bima la taifa latoa ushauri wa bure kwa wamiliki wa viwanja vya michezo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Shirika la bima la taifa latoa ushauri wa bure kwa wamiliki wa viwanja vya michezo


Na.Ahmad Mmow, Lindi
SHIRIKA la bima la taifa (NIC) licha ya kuchangia shilingi 10,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa halmashauri ya wilaya Ruangwa mkoa wa Lindi limetoa wito kwa wamiliki wa viwanja vya michezo nchini kuvikatia bima viwanja hivyo.

Wito huo umetolewa leo mjini Ruangwa na meneja wa bima wa tawi la Lindi, Azaria Mpolenkile aliyemuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo (Sam Kamanga) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi 10 milioni kwa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwaajili ya ujenzi wa  uwanja huo wa mpira hafla ambayo ilifanyika mjini Ruangwa.

Mpolenkile alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wamiliki wa viwanja vya michezo nchini kukatia bima viwanja wanavyomiliki ili kuwahakikishia fidia watazamaji wanaokuwa ndani ya viwanja hivyo wakati  wanaangalia michezo, ili wawe na uhakika wakufidiwa pindi ikitokea ajali.

Alisema ndani ya viwanja vya michezo kunakuwa na watu wengi wanaoingia kwenda kuangalia michezo Hata hivyo kunaweza kutokea ajali ambazo zinaweza kusababisha watu hao kujeruhiwa na kuwasabishia ulemavu na wengine kufa.