F TALGWU walia na Taasisi za fedha zenye mikopo ya riba kubwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TALGWU walia na Taasisi za fedha zenye mikopo ya riba kubwa


NA TIMOTHY ITEMBE BUNDA.


MWENYEKITI wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU mkoani Mara, Fanuel Karebu Kohongo  ameonyesha kusikitishwa na Baadhi ya Taasisi za mikopo ambazo zinakopesha Watumishi na kisha kuwatoza makato ya riba kubwa.

Mwenyekiti huyo alisema juzi katika kikao cha TALGWU Wilaya Bunda mkoani hapa kilichokalia ukumbi wa halmashauri ya Bunda DC kwa lengo la kujadili shuguli za uhai wa Chama na maendeleo yake na kuwashirikisha mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Kaganja Amosi Jeremia pamoja na Afisa utumishi wake Tumain Magesa.

"Ndugu mkurugenzi asilimia kubwa ya wafanyakazi hususani walimu wanateswa na mikopo ya riba kubwa ambayo inasababisha baadhi ya watumishi hao  kutoroka kazini kwasababu ya madeni wanayodaiwa na taasisi walizokopo fedha"alisema Kehongo.


Kehongo aliongeza kuwa baada ya TALGWU Taifa kuona wafanyakazi wanateseka imekuja na mango mkakati wa kuanziasha Bank yake ambayo itakuwa mkombozi kwa wafanyakazi na watakuwa wanakopa kwa riba ndogo kulingana na hisa aliyojiwekea kwa  kila mwanachama na kuongeza kuwa Banki hiyo inatarajia kuanza 2019 Januari.

Kwa upande wake katibu wa Chama hicho mkoani hapa,Mussa Gidion aliwataka watumishi wote wa serikali za mitaa kujiunga na chama hicho kwani kipo kwa mjibu wa sheria na kina lenga  wafanyakazi wote wa serikali za miataa.

Gidion alifafanua kuwa TALGWU ni chama ambacho kinatetea masilahi ya wanacha pindi inapotokea sintofahamu baina ya mwaajiri na mtumishi wa serikali hususani wanachama.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Kaganja Amosi Jeremia aliwapongeza TALGWU kwa wazo hilo na kusema kuwa Banki hiyo itakapo kamilika na kuanza shiguli zake itasaidia kupunguza baadhi ya kero ya mikopo kwa wafanyakazi.