1. Anaconda wa Kijani (Green Anaconda) Green anaconda ni nyoka mkubwa zaidi duniani anayeweza kufikia kati ya mita 6 na 9 na uzito wa kilo 250. Nyoka huyu hana sumu na kuishi katika vinamasi, mabwawa na mitoni sehemu zote za Amerika ya Kusini. Anaconda wa kike ni wakubwa kuliko wa kiume. Rangi kubwa ya miili yao ni kijani na madoa meusi na ya rangi ya chungwa.
2. Chatu mwenye kujiviringisha (Reticulated Python) Huyu ana urefu wa mita 10, hivyo kuwa nyoka mrefu zaidi duniani na ni aina kubwa zaidi ya chatu akiwa na uzito wa kilo 135.
Hupatikana katika misitu ya mvua, vichaka na mito midogo kusini-mashariki mwa Asia. Hana sumu na huishi ardhini tu.
3. Chatu wa Burma (Burmese Python) Nyoka huyu asiye na sumu ni wa tatu kwa ukubwa akiwa na urefu wa kati ya mita 5 na 7.6 na uzito wa kilo 137. Huishi katika vinamasi, misitu na mitoni kusini-mashariki mwa Asia.
4. Chatu wa Afrika wa kwenye miamba (African Rock Python) Hana sumu na ni mkubwa zaidi ya wote barani Afrika akiweza kufikia urefu wa mita 7.5 na uzito wa kilo 114. Huishi kwenye vinamasi na misitu ya Afrika Magharibi na Kati.
5. Chatu wa India (Indian Python) Hana sumu na hupatikana kusini mwa Asia akiwa na urefu wa mita 6.4na uzito wa kilo 91. Huishi msituni na vinamasi.
Ana rangi ya njano, kahawia na hudhurungi na madoa meusi, rangi zinazomsaidia kujificha popote asionekane kirahisi.
6. Chatu wa Kijivu/Zambarau (Amethystine Python) Ni mmoja wa nyoka wakubwa zaidi duniani kwa urefu na uzito, akifikisha hadi urefu wa mita 8.5 na uzito wa kilo 90. Huishi vichakani na kwenye manyasi huko Australia na Papua Guinea.
7. Anaconda wa Njano (Yellow Anaconda) Ni wa pili kwa ukubwa miongoni mwa Anaconda; ana urefu wa futi 10 hadi 15 na uzito wa kilo 60. Anapatikana Amerika ya Kusini kwenye vinamasi na mito.
8. Boa mwenye kubana (Boa Constrictor) Hana sumu, ana urefu kati ya futi 12 hadi 18 na uzito wa kilo 45. Huishi kwenye misitu ya mvua na jangwani Amerika ya Kusini na Kati. Anasifika kwa uzuri wa ngozi yake ambayo inaweza kuwa ya kahawia, nyekundu, kijani au njano.