Msanii Mrembo Mpoto amesema kwa asilimia kubwa wasanii wa Tanzania hawapendani.
Mrisho Mpoto amesema hayo baada ya kumalika kwa kikao kati ya wasanii na CCM alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
"Wasanii wa Tanzania kusema kweli hawapendani, yaani ni wanafiki kweli kweli, hapa anakuchekea lakini ndani moyoni mwake anasema hamna kitu lakini taratibu kwa sababu industry ndio inakuwa yatabadilika," amesema Mrisho Mpoto.
Kwa sasa Mrisho Mpoto anafanya vizuri na wimbo wake wa mwisho kutoa, Nimwage Radhi ambao amemshirikisha Harmonize.