F Hii ndio rangi ya mwaka 2018 katika Urembo na Mapambo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hii ndio rangi ya mwaka 2018 katika Urembo na Mapambo

RANGI ya mwaka 2018 ni purple (zambarau) inayojulikana kama UTRA VIOLET PURPLE 18-3838.

Kampuni ya Pantone Color Institute imeitangaza rangi hii ya zambarau isiyokoza sana kuwa rangi rasmi itakayotumika rasmi atika shughuli mbalimbali za mitindo , harusi, kwenye matamasha mbali mbali pamoja na mitoko tofauti tofauti.

Pantone Color Institute ni kampuni kubwa duniani inayohusika na kujikita na utafiti wa rangi katika tasnia ya mitindo (fashion) na kutoa ushauri wa matumizi ya rangi, pia saikolojia kwa wavaaji pamoja na maana zake na ilihusika kufanya  uteuzi wa rangi hizi za mwaka tangu mwaka 2000

Lakini pia Pantone hufanya kazi  kwa makampuni ya mitindo na urembo duniani  za ubunifu na uchanganyaji wa rangi ya mavazi

Rangi hii ya UTRA VIOLET PURPLE inamaanisha upekee wa kila mtu yenye kusimamia uhalisi, uelekevu na usawa kwa watu

Rangi yenye mfanano na Anga za mbali katika sayari (glaxies)  hivyo humaanisha chochote chawezekana, na yenye kutupeleka katika malengo au ndoto za baadae.

Baadhi ya watu maarufu na mashuhuri wakiwemo wasanii, wanamitindo na wanasiasa wamepambaika na mavazi yaliyosheheni rangi hii au yaliyochanywa na rangi hii katika shughuli, mitoko na maonyesho kadhaa duniani.

Kwa mwaka 2018 mapambo malimbali  yatahusika katika mchanganyiko wa rangi mbalimbali ikihusisha rangi ya Purple katika kumbi za sherehe za harusi, mwago(Sendoff), kitchen party bila kusahau kuta na sebule za nyumba za watu