Msanii wa Muziki, Matonya amefunguka kumshirikisha msanii wa Hip Hop, Fid Q kwenye wimbo wake mpya wa 'Nisulubishe'.
Matonya amesema kuwa ukizungumzia wana Hip Hop bora msanii huyo hawezi kukosa kwasababu ana radha ya tofauti na watu wengine.
"Kwenye utengenezaji wa muziki tunahitaji kupata test , tunahitaji kupata muziki mzuri, kwahiyo mziki mzuri unatengenezwa kwa njia nyingi, kumuweka pale mwanzo watu wamezoea kumuweka verse ya pili, Fid Q ana radha yake toauti na watu wengine kwahiyo nikaona akifungua alafu nikishikilia pale tunaweza tukapata combination moja kali na ndicho ambacho kimetokea hatukutaka kufanya kitu ambacho watu wamekizoea sana."
Wasanii hawa wameshawahi fanya nyimbo mbili wa kwanza ' usinikubali haraka' na mwingine 'Tax Bubu'.