F Sababu za Maumivu ya Mgongo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sababu za Maumivu ya Mgongo

Sababu za Maumivu ya Mgongo

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha maumivu ya mgongo

1. Maambukizi katika pingili za uti wa mgongo: Maambukizi katika pingili za uti wa mgongo kama vile maambukizi ya saratani ya mifupa huweza kuleta maumivu makali ya mgongo.

2. Kuvunjika kwa pingili za uti wa mgongo: Hii huweza kusababishwa na vitu mbalimbali hususani ajali ya kuanguka au kupinduka na gari.

3. Umri mkubwa: Tatizo la maumivu ya mgongo mara kwa mara huwakuta watu wazima na wazee.

4. Uzito kupita kiasi: Uzito wa mwili kupita kiasi husababisha kuelemewa kwa uti wa mgongo na hivyo kuleta mgandamizo wa pingili za uti wa mgongo na kusababisha maumivu.

5. Kukaa kwa muda mrefu: Kukaa kwa muda mrefu kama vile ofisini au madereva bila ya mazoezi hupelekea maumivu ya Mgongo.

6. Mtindo wa Maisha (Lifestyles): Mtindo wa maisha kama vile kupuuza mbogamboga na vyakula vya asili hupelekea kuwa na mifupa hafifu na hivyo ni rahisi kuathirika hata kwa msuguo mdogo tu.