Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 liloripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mgumba ameyasema hayo alipofanya ziara katika ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika.
“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii , kwenye kilimo ni vyema tukaenda na mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kiimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka.” Alisema Naibu Waziri.
Sambamba na hilo, Naibu Waziri ameitaka Tume pia kuwasilisha kwake taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika eneo la kilimo cha umwagiliaji kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano na taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uenddelezaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji Mhandisi Pascal Shayo alisema kumekuwa na ushiriki mdogo wa sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ambapo mhandisi Shayo alieleza kuwa , kukabilina na changamoto hii Tume ina Mpango wa kuanzisha miradi ya ubia baina ya seka ya ya umma na sekta binafsi ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi katika kuendeleza miundombinu ya umwagailiaji na serikali itaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake kwa kuwapatia mafunzo yanayohusu uwekezaji baina ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuwe na uwekezaji kwa ajili ya kuongeza uelewa wa masuala ya ubia na manufaa yake kwa umma.
Naibu Waziri Mgumba aliitembelea Tume ya Taifa ya Umwagailiaji akiwa na lengo la kufahamiana na watumishi kwani yeye ndiyo aliyepewa jukumu mahususi la kusimamia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.