Benson Chonya
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa Muungwana blog. Karibu ujifunze njia ya usindikaji wa mboga za majani kwa njia ya asili.
Ukaushaji wa mboga za majani ni njia ambayo inatumika sana maeneo ya vijijini lakini si vibaya ikianza pia kutumika maeneo ya mijini kwani ni njia nzuri sana. Kwa maneno mengine njia hii ni usindikaji wa mboga za majani ni mzuri sana kwani mboga hizi zitakusadia pindi patakapokuwa na uhaba wa mboga hizo.
Mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kukausha mboga za majani ni kama ifuatavyo:
- Chuma mboga nyingi katika bustani yako. Haijalishi ni mboga za aina gani.
- Hatua inayofuata ikatekate vipande vidogo vidogo.
- Baada ya hapo chemsha katika maji ya moto. Lakini jambo la kuzingatia ni kwamba chemsha mpaka ibadili rangi yake, isiwe katika hali ya ukijani.
- Mara baada ya kuchemka na kujiridhisha kwamba imeiva vizuri. Epua kisha subiri kwa muda fulani mpaka ipoe vizuri.
- Ikisha poa vizuri chukua kitu ambacho kitakusaidia kuianika mboga hiyo mpaka ikauke vizuri.
- Mara baada ya kukauka vizuri ni kwamba unaweza ukaiifadhi sehemu safi ili ije kuliwa hapo baadae.