Wana akiolojia wamefanya ugunduzi usio wa kawaida - kaburi la kasisi mmoja ambayo halijapatikana kwa miaka 4,400.
Mostafa Waziri, katibu kwenye baraza linalohusika na maeneo ya kale alitaja ugunduzi huo kama wa aina yake kwa miaka mingi iliyopita.
Kaburi hilo ambalo liligunduliwa eneo linalojulikana kama Saqqara pyramid complex mjini Cairo lina sanamu za Firauni.
Wana akiolojia wataanza kulichimba kaburi hilo leo na wanatarajia kufanya ugunduzi zaidi baadaye ukiwemo mwili wa aliyezikwa humo.