Picha ya mtandao
Mashindano ya Mpira wa Meza ya Afrika Mashariki na Kati chini ya umri wa miaka 18 yamezinduliwa rasmi Kigali nchini Rwanda ambapo zaidi ya Mataifa 6 yakishiriki katika Mashindano hayo.
Akiyafungua Mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Meza nchini Rwanda John Guruma amesema mashindano hayo yanatambuliwa na shirikisho la mpira wa meza Dunia ITTF ambapo washindi watawekwa kwenye rikodi ndani ya shirikisho hilo.
Amesema Mashindano hayo yatawapa nafasi kubwa nchi za ukanda wa afrika Mashariki kupata uzowefu mkubwa wa kushiriki mashindano ya kimataifa.
Kwa upande wake mkuu wa msafara wa timu ya taifa ya Tanzania iliyopo kwenye mashindano hayo Abubakar Khatib Kisandu amewataka Watanzania kuwa kitu kimoja na kuwaombea washinde kwenye mashindano hayo.