Mimi ndio Simba wa Tanzania - Mc Pilipili


Mchekeshaji Maarufu nchini, Mc Pilipili amesema kuwa katika  wachekeshaji Tanzania yeye ndio Simba.

Mc Pilipili amesema kuwa yeye hakujipa jina hilo isipokuwa Mungu ndiye aliyeanza kumpa.

"Mimi ni MC wa Taifa, sijui unanielewa kuna wakuu wa Mikoa mfano kaka angu Paul Makonda atakuwa hapa tu hawezi kuamua mambo ya Arusha anamuachia Mrisho Gambo, Ma Mc wengine wakubwa hapa wenyewe ndio Top sasa katika mikoa hiyo alafu mimi ndio Taifa naenda popote," alisema Mc Pilipili.

"Nataka kusisitiza kuwa katika Comedy Tanzania mimi ndio Simba mimi ndio Diamond wa Stand up Comedy nachukua jina la Simba na hilo jina sio mimi Mungu mwenyewe alianza kunipa."