AliKiba athibitisha kinywaji chake kuanza kupatikana Dar rasmi


Msanii wa muziki, Alikiba amethibitisha kuwa kinywaji chake cha Mofaya kuanza kupatikana katika mkoa wa Dar Es Salaam.

AliKiba kupitia ukurasa wake wa Instagram Kiba ameweka wazi maeneo ambayo kitakuwa kinapatikana.

"Sasa Mofaya Energy Drink zimeanza kupatikana jijini Dar es Salaam kwa Mawakala Wakuu," aliandika AliKiba.

Aliongeza kuwa watu wa mikoani wakae mkao wa kula maana kinywaji hicho kitasambaa nchini nzima.