Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa nchi ina Demokrasia na si suala la kuandamana.
Amebainisha hayo mbele ya viongozi wa dini ambapo amekutana nao leo Ikulu Dar es Salaam walipokutakana kujadili kuhusu maendeleo na changamoto za nchi.
"Demokrasia Tanzania ipo, lakini Demokrasia ina mipaka yake hakuna anayekatazwa kufanya mikutano na wanafanya na wanaendelea kufanya na nyinyi ni mashahidi, hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano mahala pake," - Rais Magufuli.
Awali Mchungaji wa KKKT, Amani Lyimo alimueleza Rais Magufuli kuwa, 'Unafanya kazi sana, lakini Baba Demokrasia,Watanzania wengi wana hofu, wengi hawadhubutu kuzungumza wana hofu, nakuomba Rais kama kuna uwezekano Baba waachie pumzi wazungumze,'.