F JKT Queens waipa kichapo Yanga Princess | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

JKT Queens waipa kichapo Yanga Princess


Kikosi cha Yanga Princess leo kimepoteza kwa kuchapwa mabao 8-1 dhidi ya JKT Queens kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League.

JKT Queens wanafanikiwa kuwafunga watani wote wa jadi baada ya kuanza na Simba Uwanja wa Karume kwa kuifunga bao 1-0 na leo wameendeleza ubabe wao kwa Yanga Princess kwa ushindi wa mabao 8-1.

Yanga Princess wanafanikiwa kuifunga JKT Queens kwani mpaka sasa baada ya kucheza michezo sita walikuwa hawajafungwa bao hata moja.

Alliance Girl wameshinda bao 6-0 dhidi ya Evergreen Queens, Baobab Queens wameshinda mabao 3-1 dhidi ya Mapinduzi Queens.