F Kamati nne za kuchapa kazi zazinduliwa na UWT | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kamati nne za kuchapa kazi zazinduliwa na UWT


Kamati ndogo ndogo nne zimezinduliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania kwa upande wa Zanzibar, leo zitakazokuwa na majukumu mbali mbali ya kufanikisha kwa ufanisi wa kazi za umoja huo kwa mwaka 2019/2020.

Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi amezungumza mara baada ya uzinduzi huo na kuzitaja kamati zilizozinduliwa kuwa ni pamoja na Kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha, Kamati ya Mawasiliano kwa Umma, Kamati ya Elimu,Malezi na Mafunzo pamoja na Kamati ya Mahusiano na Taasisi za Wanawake ndani na nje ya Nchi.

Alisema kuwanzishwa kwa kamati hizo ni matarajio makubwa zaidi ni kuwafikia Wanawake na Vijana pamoja na makundi mbali mbali yaliyopo katika jamii na watoto ili kushinda Uchaguzi ujao mwaka 2020.

“Wanawake ni Jeshi kubwa tena la ukombozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nasaha zangu kwenu ni kwamba tutumie nafasi hii kuhakikisha tunawafikia wanawake wote hasa waliopo Vijijini na Pembezoni kwa nia ya kuwaweka karibu na kufanya nao shughuli zetu za kisiasa.

Katika maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo aliwasisitiza Wajumbe wote wa Kamati hizo kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya UWT pamoja na CCM kwa ujumla.