Hans Van Pluijm ambaye ni Kocha Mkuu wa Azam FC na amefanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa amewapa mbinu kali Simba ili waweze kuwaua wapinzani wao mapema kwenye hatua ya makundi.
Kocha huyo amesema anaamini Simba wananafasi kubwa ya kupata matokeo iwapo wataamua kushirikiana na ushindani kwenye hatua ya makundi ni mkubwa hasa ukizingatia kundi ambalo wamepangwa wana nafasi ya kupenya iwapo hesabu kubwa zitakuwa ni kushinda.
"Ushindani kwenye hatua ya makundi hasa wa Ligi ya Mabingwa sio sawa na huu wa kwenye Ligi Kuu Bara, nafasi pekee ambayo itawasaidia kuweza kupata matokeo ni kucheza wakiwa ni timu na siyo kumtegemea mchezaji mmoja'' alisema Pluijm
Hata hivyo amesema kuwa kundi lao lina timu nzuri hawapaswi kubeza na timu zote zimejipanga na wajue kwamba kipindi cha kwanza kwa wapinzani huwa ni za ushindani hivyo wanapaswa kuwadhidibiti mapema na kupata matokeo ya haraka.