Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa moja ya vitu anavyojivunia kwa Mbosso ni mafanikio yake.
Mbosso ambaye yupo chini ya lebo ya Diamond Platnumz 'WCB' amefanya vizuri kwenye show ya Wasafi Festival Mombasa nchini Kenya kitu ambacho Diamond anaeleza kujivunia.
"Naamini Kupitia Story ya Maisha yako itawatia Moyo na Kuwapa Nguvu Vijana wengi Kuwa Usipokata tamaa, ukijituma, kuheshumu na Kumuomba sana Mwenyez Mungu basi ipo siku nae Atakufikishia ndoto yako na Kukukuza, mafanikio yako ni faraja kubwa sana Kwangu," amesema Diamond.
Usiku wa January 27, 2018 Mbosso naye akatambulishwa WCB na hapo hapo akatoa wimbo wake wa kwanza uitwao Watakubali. Huyo ndiye msanii wa mwisho kusaini kwenye lebo ya WCB.