F Mradi mkubwa wa Umeme kuiunganisha Tanzania na Kenya waanza kutekelezwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mradi mkubwa wa Umeme kuiunganisha Tanzania na Kenya waanza kutekelezwa


Mradi mkubwa wa umeme unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) ambao utaiwezesha nchi kununua au kuuza umeme katika nchini za Afrika umeanza kutekelezwa ambapo kwa sasa mradi wa kuunganisha umeme katika nchi za Kenya na Tanzania umeanza.

Mradi huo unafahamika kwa jina la Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP) ambapo kutakuwa na hatua mbalimbali za kuutekeleza mradi huo uliogawanywa katika hatua nne za utekelezaji wake huku TANESCO ikifafanua umuhimu na faida lukuki za mradi utakapokamilika na kwa sasa wakandarasi wapo kazini na kanzi imeanza kufanyika.

Kwa mujibu wa TANESCO awamu ya kwanza itakuwa ni kuziunganisha nchi zilizopakana na Tanzania kuwa na umeme wa uhakika huku awamu ya pili ya mradi huo ukihusisha nchi za Tanzania na Zambia (ZTK) ambao nao tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara imeanza.Akiuzungumzia mradi huo jana jijini Arusha, Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye, amefafanua mradi huo wanaamini utakamilika kwa wakati kama ambavyo wamekubaliana na wakandarasi ambao tayari kazini na vifaa vyote muhimu vimefika na kazi ya kusimika nguzo imeanza.

"Jumla ya mradi wote una umbali wa kilometa 510 lakini kwa upande wetu Tanzania tunazo kilometa 414 na upande wa Kenya nao wanakilometa 96.Kwa upande wetu tunakwenda vizuri kwani kila kipande cha ujenzi wa mradi kuna mkandarasi wake na kila mmoja yupo hatua mbalimbali za ujenzi.Kupitia watalaam wetu tumekuwa tukifuatilia hatua kwa hatua na wakati huo huo wapo watalaamu wengine ambao nao wanafanya kazi hiyo hiyo kuhakikisha kila kinachofanyika kimezingatia mahitaji na vigezo vya viwango vya ubora,"amesema Mhandisi Kigadye.

 Pia kutakuwa na sehemu ya tatu ambayo ni Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambako kuna kilomita nyingine 624, hivyo baada ya kukamilika kwa mradi Tanzania itakuwa imekamilisha ule mkongo wa msongo wa Kilovoti 400.Lengo kuu la kuunganisha nchi yetu na ukanda nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia maana yake ni kuifanya Tanzania kuingia kenye mfumo wa umeme ambao utahusisha nchi mbalimbali za Afrika.